MIKAKATI YA KUKUZA UWEKEZAJI NCHINI
1. Itaanzisha Kituo Maalum cha kuhudumia na kuwezesha wawekezaji vijana (Youth Investors Resource Centre).
2. Kuanzishwa kwa programu maalum ya kuwezesha wawekezaji vijana kubuni na kuanzisha uwekezaji wa viwanda nchini kote.
3. Itasogeza huduma za Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi kufikia kila Mkoa ifikapo mwaka 2028.
4. Serikali itashirikiana na sekta binafsi kujenga miundombinu ya uwekezaji wa viwanda nchi nzima
5. Serikali itatunga na kuanzisha vituo vipya vya kiuwekezaji ili kuongeza uimara wa uwekezaji nchini na mvuto wa Tanzania kwa wote wenye mitaji huko duniani.
6. Serikali itaanzisha jukwaa rasmi ya kukutana na wawekezaji wote kila miezi mitatu kufanya tathmini ya mwenendo wa uwekezaji, kusikiliza changamoto na kupokea maoni na mapendekezo ya maboresho mbalimbali.
7. Serikali itasogeza huduma za Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi kufikia kila mkoa ifikapo mwaka 2028.
8. Kuweka mazingira maalum ya kuvutia uwekezaji katika kuzalisha bidhaa tunazoagiza nje na ambazo tunaagiza sana kutoka nje.


