Mradi wa umeme wa Kilovoti 132 Tabora wabakiza asilimia 5 kukamilika

HomeKitaifa

Mradi wa umeme wa Kilovoti 132 Tabora wabakiza asilimia 5 kukamilika

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limesema ujenzi wa miundombinu ya umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi unaofanywa na kampuni tanzu ya ETDCO umefikia asilimia 95 huku umeme ukitarajiwa kuwashwa mwishoni mwa mwezi huu wa Mei, 2025.

Mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 40 utawaondolea changamoto ya umeme wananchi wa mkoa wa Tabora, wilaya ya Urambo na Kaliua.

Licha ya kuwa mradi huo utasaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika pia mradi unatekelezwa na wataalamu wazawa jambo ambalo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha wazawa wanapewa fursa katika uendeshaji na utekelezaji wa miradi.

 

error: Content is protected !!