Utaratibu wetu wa maisha unazunguka saa 24 kwa siku, saa 12 za jua na saa zingine zilizobakia ni wakati wa usiku.
Lakini, Je! Unajua kwamba kuna maeneo ulimwenguni ambapo jua halizami kwa kwa zaidi ya siku 70?
Hapa chini ni orodha ya maeneo 6 duniani ambapo jua kwa kipind fulani huwa halizami:
Norway
Norway, iliyoko kwenye mzunguko wa Aktiki, huitwa ‘Ardhi ya Jua la Usiku wa Manane,’ ambapo kuanzia Mei hadi mwishoni wa Julai, jua halizami kabisa.
Hii inamaanisha kuwa kwa karibu kipindi cha siku 76, jua huwa halizami. Katika eneo la Svalbard, Norway, jua linaangaza mfululizo kutoka Aprili 10 hadi Agosti 23.
Nunavut, Canada
Nunavut iko karibu digrii mbili juu ya mzunguko wa Aktiki, katika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Canada.
Iceland
Iceland ni kisiwa kikubwa zaidi barani Ulaya baada ya Uingereza, na pia inajulikana kwa kuwa nchi ambayo haina mbu.
Wakati wa majira ya joto, usiku huwa wazi huko Iceland yaani hakuna giza, na wakati wa mwezi wa Juni, jua halizami.
Ili kuona jua la usiku wa manane katika ubora wake likiwa linang’aa kweli, unaweza kutembelea jiji la Akureyri na Kisiwa cha Grimsey kwenye mzingo wa Aktiki.
Barrow, Alaska
Mahali hapa pana karibu miezi miwili ya jua kwa saa 24, wakati wa msimu wa baridi, mahali hapo huona jua takriban siku 30 mfululizo. Kuanzia mwishoni mwa Mei hadi mwishoni mwa Julai, jua halizami hapa, ambalo baadaye hufidiwa kutoka mwanzoni mwa Novemba kwa siku 30 zijazo, ambapo jua halichomozi, na hujulikana kama usiku wa polar au ‘polar night’. Hii inamaanisha pia kuwa nchi inabaki kwenye giza wakati wa msimu wa baridi kali. Eneo hilo pia ni maarufu kwa milima iliyofunikwa na theluji zenye kupendeza. Mahali hapa panaweza kutembelewa katika majira ya joto au baridi.
Finland
Ardhi yenye maelfu ya maziwa na visiwa, sehemu nyingi za Finland hupata kuona jua moja kwa moja kwa siku 73 tu wakati wa msimu wa joto.Wakati huu, jua linaendelea kuangaza kwa karibu siku 73, huku wakati wa msimu wa baridi, eneo hilo halioni mwanga wa jua.
Pia ni moja ya sababu kwanini watu hapa hulala muda mfupi msimu wa jua, zaidi ya msimu wa baridi.
Uswidi
Kuanzia mwanzoni mwa mwezi Mei hadi mwishoni mwa Agosti, Uswidi huona jua likitua usiku wa manane na kuchomoza kuanzia saa 10 alfajiri.
Hapa, kipindi cha jua kuwepo mara kwa mara kinaweza kudumu hadi miezi sita kwa mwaka.