Panya Road wasimulia wanavyoiba

HomeKitaifa

Panya Road wasimulia wanavyoiba

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limeendelea kuisimamia operesheni maalum kali na msako wa mtaa kwa mtaa dhidi ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu panya road na mpaka tarehe 6.5.2022 limewakamata wahalifu 31 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uporaji baada ya kuvunja nyumba, kujeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya nyumbani .

Mmoja wa watuhumiwa hao ni kijana Yunus Jafar (20) ambaye amesimulia jinsi wanavyofanya uhalifu.

“Matukio yetu ya kiuhalifu huwa tunafanya usiku, tunakutania Mtaa wa Msumbiji (Chanika) Mnara wa Voda, suala la kuiba huwa halipangwi Watu wanatoka na kuingia kila nyumba baada ya hapo kuna Mtu anachukua vile vitu na kuondoka navyo na kisha vinauzwa mnagawana hela”

“Anayetutuma ni Rafiki yetu yeye ni mkubwa kuliko sisi, tukiuza mali tunagawana kinachopatikana, Elfu 50 hadi Laki 1, Wazazi wangu hawafahamu ninachokifanya, kilichonishawishi kufanya uhalifu ni marafiki, mapanga alikuja nayo Rafiki yangu yalikuwa kwenye mabegi” alisema Yunus.

Katika mahojiano ya kina, Jeshi la Polisi limebaini kuwa watuhumiwa hao wamehusika katika vitendo hivyo vya kihalifu na kuonesha baadhi ya vitu walivyoiba zikiwemo TV 12 na simu za mkononi 4. 

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo na halitasita kuwakamata ambao wamekuwa wakipokea mali mbalimbali za wizi zinazotokana na matukio ya kihalifu na Jeshi la Polisi halitasita kuwafikisha kwenye vyombo vingine vya kisheria.

error: Content is protected !!