Pesa za ujenzi zaanza kuwa za moto, Afisa manunuzi atumbuliwa

HomeKitaifa

Pesa za ujenzi zaanza kuwa za moto, Afisa manunuzi atumbuliwa

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amemsimamisha kazi kwa kipindi cha miezi miwili Afisa manunuzi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga anaejulikana kama Zakaria Awe kwa kushindwa kuwajibika katika suala la ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani humo.

Pia Mkuu wa Mkoa amewaweka chini ya uangalizi wa Mkuu wa Wilaya wakuu watatu wa Idara ambao wameshindwa kuhimiza suala la ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kutokana na fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Pesa hizo zilizotolewa kwaaajili ya kuhakikisha vyumba vya madarasa vinajengwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza 2022 waanze shule kwa pamoja nchini kote.
Maagizo hayo ya Mkuu wa wilaya yalitolewa wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo katika shule yta Sekondari Kishapu. Mkuu wa Mkoa aligundua mapungufu katika ujenzi huo ikiwemo ucheleweshwaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kutokana na kutonunuliwa kwa vifaa.

Mkuu wa Mkoa amesema “Kuna watu ambao mnatuchelewesha kazi, mnatuwekea kiwingu mbele ili tusimalize kazi zetu, sikubali kwa maana hiyo kuanzia sasa Afisa manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya utakaa pembeni mpaka Desemba tutakapomaliza kazi ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa”.

Pia mkuu wa Mkoa Sophia Mjema amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa Wilaya aweke mtu mwingine atakaendana na kasi yao “Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wekeni mtu mwingine atayekwenda na kasi yetu, huyu asitucheleweshe kazi zetu mpaka leo eneo la ujenzi hakuna hata nondo naambiwa eti wewe hujaamua saruji hakuna sasa kwa hili tutamaliza kazi hii kwa wakati kweli? Kaa pembeni”.

error: Content is protected !!