Rais Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani Ruvuma na kuhutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano katika Uwanja wa Majimaji.
Akizungumza na umati huo, Rais Samia amesema lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua na kujionea maendeleo lakini pia kuona changamoto zinazowakabili wananchi wa Ruvuma na kuzitafutia ufumbuzi.
“Nilitumia fursa hii kutatua miradi ili kukagua miradi inayoendelea na kuzindua mingine iliyokamilika”amesema Rais Samia.
Baadhi ya miradi aliyoizindua ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu, Soko la Madini ya Vito na Dhahadu Tunduru, Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay na Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.