Waandaji wa tuzo za AFRIMMA wamemtunukua Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tuzo ya Uongozi Bora kwa mwaka 2022 kutokana na mchango wake katika kukuza na kuboresha tasnia ya sanaa na burudani.
Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka kwa kiongozi mwenye mchango mkubwa kwenye jamii imebainisha mambo makubwa aliyoyafanya Rais ikiwa ni pamoja na kubadili sheria za sekta hiyo pamoja na kushiriki uandaaji wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour.
Mamlaka hiyo imempongeza Rais kwa kubadili mfumo wa hatimiliki ambao unakuza uwezo wa kiuchumi wa wasanii.
View this post on Instagram