Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi uwepo wa goli la mama katika mashindano wa kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Ametoa ahadi hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii alipokuwa akiipongeza timu ya Zanzibar Heroes kwa kufanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Ninaipongeza Zanzibar Heroes kwa kufanikiwa kufika hatua ya fainali ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Mmejitoa, mmejituma na sote tunajivunia safari yenu hadi sasa.
Mchezo huu wa fainali ni nafasi ya kipekee kwenu kuandika historia, nasi tuko nyuma yenu kuwaunga mkono.… pic.twitter.com/IUhA5I7h9A
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) January 13, 2025