Rais Samia: Hongera Rais Putin

HomeKimataifa

Rais Samia: Hongera Rais Putin

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, kuadhimisha Siku ya Ushindi ya Mei 9.

Katika ujumbe wake uliochapishwa kwenye ukurasa wa X, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa siku hiyo kama ishara ya ujasiri, mshikamano, na kujitolea kwa watu wa Urusi katika harakati za kupigania uhuru na amani.

Ameeleza kuwa ushindi wa miaka 80 iliyopita katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia ni urithi wa kihistoria unaoendelea kuhamasisha mataifa yote kudumisha amani, haki, na ushirikiano.

Aidha, Rais Samia amesisitiza thamani ya urafiki kati ya Tanzania na Urusi, unaojengwa juu ya heshima na mshikamano wa pande zote mbili.

error: Content is protected !!