Rais Samia Suluhu awasha moto Mamlaka ya Bandari

HomeKitaifa

Rais Samia Suluhu awasha moto Mamlaka ya Bandari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mkurugenzi Mkuu wa bandari na mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU wakaisome vizuri ripoti iliyotolewa na mkaguzi mkuu CAG ili kuchukua hatua kwa ubadhirifu wa fedha uliotokea katika Shirika la Bandari. Hayo yalisemwa leo na Rais Samia alipoenda kuzindua gati 1 hadi 7 katika bandari ya Dar es Salaam.

“Mkurugenzi wa TPA, Waziri na TAKUKURU mpo, naamrisha ripoti ya CAG mkaisome, halafu mchukue hatua, fedha nyingi sana imepotea watu tunachekeana tu, na bado waliotajwa kwenye ripoti bado wapo maofisini wanaendeleza wizi,” alisema Rais Samia

Kuna mapungufu mengi Rais Samia ambayo ameyaiinisha katika shirika hilo la bandari ikiwemo kuchezewa kwa mifumo ya bandari, kutokana na mifumo hiyo kuchezewa inapelekea kupitisha mizigo ambayo haijalipiwa huku ikionyesha imelipiwa. Lakini pia kutokana na ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG pesa nyingi zilitumika kulipa mashirika ambayo yalikua yatoe huduma na hayakutoa ikiwemo utengenezaji wa mifumo mbalimbali ya kusaidia utendaji bandari.

“Wafanyakazi wa TPA hasa wa sehemu za hesabu wamechezea mifumo, kiasi ambacho ukisoma mfumo unaonesha mizigo inayoshushwa imelipiwa na mageti yanaruhusu mizigo kutoka, ukweli ni kwamba mizigo haijalipiwa, Mkurugenzi kuwa macho” alisema Rais Samia Suluhu

Rais Samia alisema alipata fununu uwepo wa nyufa katika gati namba 1 na alipomuuliza waziri alikiri kuwa zilikuwepo ila zimezibwa, Kulikua na marekebisho ya tagi za kuvutia meli ambayo gharama zilisema mategenezo yake ni bilioni 6.6 kwa kila moja wakati kulikua na uwezo wa kufanya zikatengenezwa hapa hapa nyumbani kwa shilingi milioni 700 kila moja kwahiyo akaomba zijengwe chelezo ili meli zitengenezwe hapa nyumbani.

Lakini pia kuna suala la ujenzi wa matanki ya mafuta ambao Rais anasema alipata nao mashaka kutokana na gharama za ujenzi wa matanki hayo, ndo maana nikasema uache mara moja na kama mnataka kuanza kujenga basi tenda itangazwe upya.
“Kulikuwa na mradi wa ujenzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta, mamilioni kadhaa ya pesa yametengwa, nikamwambia Mkurugenzi Mkuu, nimekuleta hapa ulinde ‘interest’ za Taifa, huu mradi unanitia wasiwasi na naomba uusimamishe” alisema Rais Samia Suluhu Hassan.

error: Content is protected !!