Rais Samia :Tamasha la Kizimkazi linachochea maendeleo na kudumisha mila

HomeKitaifa

Rais Samia :Tamasha la Kizimkazi linachochea maendeleo na kudumisha mila

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amepongeza juhudi za Tamasha la Kizimkazi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kudumisha mila na desturi za Watanzania. Akizungumza katika kilele cha tamasha hilo, Rais Samia alibainisha kuwa tamasha hilo lina mchango mkubwa katika kuwajumuisha wananchi na kuimarisha udugu.

“Tumekusudia kutumia tamasha hili kama jukwaa la kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Lengo kuu ni kuwaleta watu pamoja, kudumisha udugu wetu na kulinda mila na desturi zetu,” alisema Rais Samia.

Tamasha la mwaka huu lilijumuisha matukio muhimu kama vile uzinduzi wa miradi mipya, uwekaji wa mawe ya msingi, mafunzo kwa vijana, michezo, na maonyesho ya tamaduni mbalimbali za Tanzania. Rais Samia alielezea furaha yake kwa kushiriki katika matukio hayo na kupongeza wadhamini wa tamasha kwa mpangilio mzuri wa shughuli.

“Mafunzo ya muda mfupi yalitolewa kwa vijana 605, na yaliangazia ujasiriamali, utalii, kilimo, mifugo, uvuvi, na sanaa,” aliongeza Rais Samia.

Akiendelea na hotuba yake, Rais Samia alisema kuwa serikali imekusudia kutumia matamasha kama haya katika kudumisha utamaduni, mila, na desturi za Taifa, huku ikichangia ukuaji wa uchumi kwa jamii.

error: Content is protected !!