Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka jamii nchini kulinda na kuendeleza mila, tamaduni na desturi zilizo nzuri na kuwarithisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Rais ametoa rai hiyo wakati akihutubia kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi katika Kijiji cha Kizimkazi kusini Unguja Zanzibar.
Amesema kwa sasa dunia ipo kwenye zama za utandawazi hivyo mikakati thabiti inahitajika kuhakikisha jamii inalinda mila, tamaduni na desturi zilizo nzuri ili zisipotee na kuachana na zile mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji.
Katika kilele cha tamasha hilo Rais Samia ametembelea mabanda ya wajasiriamali na kujionea bidhaa wanazozalisha, kuzindua majengo mbalimbali, kupokea maandamano ya vijana takribani 250 na kushuhudia maonesho ya asili ya Shomoo.
Miongoni mwa malengo ya tamasha hilo ni pamoja ba kujenga kituo kikubwa cha afya kitakachowahudumia wana Kizimkazi na wakazi wengine wa maeneo ya jirani, kutangaza fursa za kiuchumi zinazopatikana Kizimkazi kama vile utalii, uchumi wa bahari/uchumi wa bluu na uvuvi.