Ifahamu kwa undani chanjo ya korona ya ‘Janssen’ ya kampuni ya Johnson & Johnson

HomeElimu

Ifahamu kwa undani chanjo ya korona ya ‘Janssen’ ya kampuni ya Johnson & Johnson

Ni wazi wengi wanaitambua kampuni hii kwa utengenezaji wa mafuta na sabuni za watoto. Mbali na vipodozi kampuni hiyo pia inazalisha vifaa tiba na dawa zitumikavyo za binadamu.

Johnson & Johnson wanatengeneza dawa za saratani, vifaa tiba na dawa za magonjwa ya akili. Mataifa mengi duniani kwa sasa yanazalisha chanjo za UVIKO-19, lakini utendaji kazi wake umegawanjika katika makundi manne, nayo ni;

  • Inactivated Vaccine – Chanjo hizi hutumia kirusu butu, kirusi kilichotolewa uwezo wa kusababisha maradhi kwa binadamu. Virusi hivi hukuzwa katika mazingira maalumu kisa kuchanganya na kemikali maalumu na kuchomwa kwenye mwili wa mtu kama chanjo. Virusi hivi kazi yake ni kusaidia kinga mwili kupambana na magonjwa.
  • Protein-basaed vaccines – Chanjo hii hutumia chembechembe za protini ambazo zina uwezo wa kuiga tabia za kirusi cha korona. Chembe hizo za protini zinasaidia chembe hai za mwili kuzalisha kinga dhidi ya kirusi cha korona.
  • Viral Vector vaccines – Chanjo hutumia kirusi butu kupeleka vinasaba vyenye kinga kwenye seli/chembe hai za mwili ili kupambana na magonjwa. Yaani, hii hutoa msaada kwa seli ili kupambana na magonjwa.
  • RNA and DNA – Wataalamu wa Injia ya vinasaba hutengeneza DNA na RNA bandia ambazo zina uwezo wa kuzalisha protini maalum kwenye mwili wa binadamu na kisha hupelekea kutoa msaada ya kupambana na kirusi au ugonjwa ndani ya mwili.

Sasa je, kati ya aina hizo za chanjo, chanjo ya Janssen iko kundi gani na faida na hasara zake ni zipi?

Chanjo ya Janssen ni viral vector, hutumia kirusi maalumu kinachokuzwa maabara, kirusi hiki hakina madhara na kazi yake kubwa ni kusafirisha tu kinga dhidi ya maradhi kwenye seli ya mwili. Hawa virusi (vector) wameondolewa uwezo wa kukua na kudawanyika wanapotea baada ya kazi yake kuisha.

Chanjo ya Janssen huchomwa mara moja tu kwenye msuli wa juu ya mkono. Inashauriwa kuchomwa kwa mtu kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Upo uwezekano wa kupata matokeo yafuatayo baada ya kupiga chanjo hii; maumivu, kuvimba, uchovu, kichwa kuuma, misuli kuuma, homa, kichefuchefu na miwasho. J&J kupitia tovuti yao imesema kuwa dalili hizi ni siku ya moja au mbili baada ya chanjo, ni dalili za kawaida kwa kuwa mwili wako unatengeneza kinga na zitaondoka ndani ya siku chache.

Kuhusu usalama wake

Hali ya kuhisi vibaya baada ya chanjo inadumu ndani ya siku saba tu , na sio hatari kiasi cha kusababisha madhara makubwa.
Hali ya kuhisi vibaya inatokea kwa watu wenye umri kati ya 18 – 59 tofauti na wale wenye miaka zaidi ya 60.

Chanjo ya J&J imeonesha ubora wa kupambana na kirusi cha korona kwa 66%. Chanjo ilijaribiwa kwa watu ambao hawajawahi kuugua korona, na watu hao walithibitika kuwa na kinga zaidi wiki mbili baada ya chanjo.

Chanjo hii imethibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia kuumwa zaidi, pia kupunguza uwezekano wa kifo kwa mtu anayeugua. Chanjo ilionesha kuwa hakuna mtu aliyelazwa hospitali wiki nne baada kupata kuchomwa.

Siku 28 baada ya kupata chanjo ya Janssen, ilionekana kuwa na uwezo wa 66.9% dhidi ya magonjwa mengine hatarishi na 93.1% dhidi ya kumfanya mtu aliyepata korona kulazwa hospitali.

Vipi kuhusu mama mjamzito?

WHO inashauri chanjo ya Janssen kwa mjamzito endapo tu chanjo haitomfanya mama mjamzito akapata madhara yeye na kiumbe kilicho ndani. Ili mjamzito apate chanjo, lazima wapewe taarifa kuhusu athari ambazo zinaweza kujitokeza. Bado hakuna tafiti za kutosha kushauri moja kwa moja mama mjamzito apigwe chanjo, ingawa mimba ni moja ya sababu inayomuweka mwanamke hatarini kupata korona.

Watu gani hawashauriwi kuchomwa chanjo hii?

Watu wenye mzito (allergy), mtu mwenye joto la mwinyi kuanzia 38.5%, watu chini ya miaka 18, ingawa sababu hii bado inafanyiwa utafiti zaidi.

error: Content is protected !!