WAKAZI: Wakristo tuache unafki

HomeKitaifa

WAKAZI: Wakristo tuache unafki

Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Tanzania, Wakazi ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha TCRA kuifungia video ya wimbo wa ‘Mtasubiri” ya Diamond na Zuchu huku akisema kwamba haoni ubaya wa video hiyo na kuwataka wakristo kuacha unafki.

Wakazi ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa yeye ameona ni ubunifu umetumika kwenye video hiyo na hakuona sababu ya kuifungia, pia amewashangaa wasanii wenzake kukalia kimya suala hilo na kuhoji kama ni uoga au wamefurahishwa na kitendo hicho.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Webiro Wassira #TheLeader (@wakazi)

Baada ya kuandika hivyo watu wengi waliweka maoni yao na mmoja wao ni mrembo Silvia Sebastian Bebwa mshindi wa taji la Miss Tanzania 2019, ambaye aliunga mkono hoja ya Wakazi.

Miss Tanzania 2019, Silvia Bebwa akiunga mkono hoja na Wakazi.

error: Content is protected !!