Sabaya na wenzake kukata Rufaa

HomeKitaifa

Sabaya na wenzake kukata Rufaa

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanatarajia kukata rufaa baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Sabaya na wenzake wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

 > Sabaya alivyoachiwa huru na Mahakama kwa kujifanya Afisa usalama

Hukumu hiyo iliyotolewa jana Ijumaa Oktoba 15, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake pasi na shaka.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo, Wakili wa Sabaya na wenzake, Mosses Mahuna amesema hawajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa kwa sababu ina mapungufu mengi.

error: Content is protected !!