Samaki aliyevuliwa kwa siri auwa 6 Zanzibar

HomeKitaifa

Samaki aliyevuliwa kwa siri auwa 6 Zanzibar

Jumla ya watu 6 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 11 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Micheweni, watu hao wabasadikika kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Msuka Taponi, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskani Pemba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Said Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda Juma alisema samaki huyo alivuliwa kwa siri Novemba 24 mwaka huu wakati kwa mujibu wa sheria samaki huyo haruhusiwi kuvuliwa ila walimvua kwa siri na kwenda kumtoa sumu kwa namna wanavyojua.

“Kwa Sababu inadaiwa alivuliwa tarehe 24, wakamchemsha na kumlaza kisha tarehe 25 wakamla, Madhara yakaanza kujitokeza tarehe 26 na 27 kwa watu watano kufariki na jana tarehe 28 asubuhi amefariki mzee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70”.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu, Katika salamu hizo za rambirambi alizozitoa jana Novemba 28 alieleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzitaka familia za marehemu kuwa na subira na ustamilivu kjatika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

error: Content is protected !!