Simon Msuva akutwa na Korona

HomeKimataifa

Simon Msuva akutwa na Korona

Timu ya Wydad Casablanca ya Morocco itamkosa nyota wake Simon Msuva wakati mtanange dhidi ya Shabab Al-Sawalem siku Ijumaa katika dimba la Ahmed Shoukry katika mji za Zamamra kutoka na kuugua UVIKO-19.

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Simon Msuva hato kuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kukutwa UVIKO-19. Msuva alipimwa baada ya kuwasili Morocco, vipimo vikaonesha kuwa ameambukizwa UVIKO-19, hivyo atawekwa karantini kwa siku kadhaa hadi pale hali yake itakapotengemaa.

Inasemekana kuwa Simon Msuva alipata virusi hivyo baada ya kuwasili Tanzania kuitumikia timu yake ya Taifa kwenye mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini Qatari 2022, dhidi ya DRC, na mchezo dhidi ya Madagascar uliochezwa jijini Antananarivo.

Wydad itakuwa ugenini siku ya Ijumaa tarehe 19 November ikikipiga dhidi ya Shabab Al – Sawalem.

error: Content is protected !!