Songea namba 7 miji inayokua kwa kasi zaidi duniani

HomeKitaifa

Songea namba 7 miji inayokua kwa kasi zaidi duniani

Ifikapo mwaka 2025 idadi ya watu duniani inakadiriwa itafika bilioni 8.1. Katika kipindi hiki miji mingi barani Ulaya imekuwa ikikua kwa kasi ndogo, lakini baadhi ya miji hasa katika mataifa yanayokua kiuchumi ukuaji wa miji yake  ni wa kasi sana.

Kwa mujibu wa mtandao wa “Visual Capitalist” uliotoa utafiti huu kwa msaada mkubwa wa takwimu kutoka Umoja wa Mataifa umeanisha miji 20 duniani inayokuwa kwa kasi ambapo wameangalia kigezo cha kukua kwa uchumi katika wastani wa kila mwaka kuanzia 2020 – 2025.

Katika orodha hiyo miji 17 kati ya 20 ambayo inakuwa kwa kasi duniani inapatikana barani Afrika, huku miji minne lati ya hiyo inapatikana nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa Mkoa wa Ruvuma una idadi ya watu 1,376,891 huku Wilaya ya Songea ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu inayokadiriwa kuwa 203,309.

Mkoa wa Ruvuma ilipo wilaya ya Songea ndio kinara katika  uzalishaji wa mazao cha chakula (hasa mahindi), kuliko mkoa mwingine wowote hapa Tanzania. Zaidi ya asilimia 70% ya ardhi ya Songea inalimwa mahindi.Ifuatayo ni miji 10 inayotarajiiwa kukua kwa kasi zaidi kuanzia 2020 – 2025.

1. Gwagwalada – Nigeria, Mji huu unakuwa kwa kiwango cha 6.46% kwa mwaka.
2. Kabinda – DRC, 6.37%
3. Rupganj – Bangladesh 6.36%
4. Lokoja – Nigeria 5.93%
5. Uige – Angola 5.92%
6. Bunjumbura – Burundi 5.75%
7. Songea- Tanzania – 5.74%
8. Xiongan – China 5.69%
9. Potiskum –  Nigeria 5.65%
10. Bunia – DRC – 5.63%

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Benki ya Ulaya, idadi ya watu barani Afrika inakuwa kwa kasi zaidi kuliko mabara yote kwa ujumla. kwa mfano ukichukua kiwango cha Kusini mwa Jangwa la Sahara pekee, kiwango cha wanawake kujifungua ni 4.6 ukilinganisha na 2.4 ambacho ni kiwango cha dunia nzima.

error: Content is protected !!