Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa leo Desemba 2, na uongozi wa kamati wa Miss Tanzania kwenye ukurasa wao wa Instagram, wameeleza hayo.
“Kesho Tarehe 3 December 2021 ndio mwisho wa kuingia kambi ya Miss World baada ya nchi nyingi kupata changamoto ya kuchelewa kupata Visa ya Marekani kwa wakati. Miss World wakaongeza muda na kuruhusu hadi ikifika hiyo kesho iwe mwisho,”
“Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu yanafanyika nchini Puerto Rico , na Puerto Rico ni ‘territory ‘ ya marekani hivyo utahitaji visa ya Puerto Rico moja kwa moja ama utahitaji kua na Visa ya Marekani hata kama hutaingia marekani ili kuweza kuingia Puerto Rico haswa kwa nchi za Africa, maana hamna Embassy wala consulate hata moja barani Africa,”
““Hii ndio kusema kwa mwaka huu haitawezekana tena. Hata hivyo mwisho wa mashindano ndio mwanzo wa mashindano yajayo. Tunashukuru sana wadau wetu Miss World kwa jitihada kubwa na kuhakikisha hadi tunapata appointment mapema badala ya Januari, Serikali ya Puerto Rico ambao ndio wenyeji wa mashindano, umoja wetu wa ‘country coordinators’ dunia nzima imetufanya tumekua kitu kimoja badala ya kua washindani,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Hivi karibuni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania waliwasilisha jina la mshindi wa pili Juliana Rugamisa badala ya mshindi wa kwanza Rose Manfere ili aende kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya urembo wa Dunia jambo lililozua mtafaruki ingawa BASATA walimeilekeza kampuni ya “The Look” inayohusika na mashindano hayo kumpelekea jina la Rose lakini tamko hilo halikutekelezwa.