Tanzania, Uingereza kuboresha uhusiano wa kibiashara

HomeKimataifa

Tanzania, Uingereza kuboresha uhusiano wa kibiashara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza dhamira na msimamo wa Tanzania katika kuboresha uhusiano wa kibiashara na Uingereza.

Rais Samia aliyazungumza haya wakati akizungumza na Mwakilishi wa Uingereza Lord John Walney Glasgow nchini Uskochi. Rais Samia alisema kuwa, Tanzania na Uingereza zimekuwa na uhusiano mzuri kwa kipindi kirefu sasa, na Uingereza ni moja ya nchi zinazoongoza kufanya biashara na Tanzania.

Kwa upande wake Lord Walney amesema kuwa kukutana na Rais Samia kumerahisisha kazi sana kazi yake, kwani ametambua vipaumbele vilivyowekwa na Tanzania kwenyed dira yake ya maendele na hivyo itamsaidia sana kujua na nama ya kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Uingereza. Lord Walney amesema kuwa, taarifa kutoka kwa Rais Samia itamfanya ashawishi Waingereza wengi wenye ndoto ya kuwekeza Tanzania.

error: Content is protected !!