Diwani ataka mabadiliko kampeni ya tohara

HomeKitaifa

Diwani ataka mabadiliko kampeni ya tohara

Diwani wa Mwankulu Manispaa ya Mpanda, Kapili Katani amelalamikia kampeni inayofanywa na watoa huduma wa tohara kwa wanaume kwa kuwataka wanawake kuwakataa wanaume wasiotahiriwa, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani Katani anasema kampeni hiyo inakiuka haki za binadamu kwa kuwa tohara ni suala la hiari.

Katani anasema ni vema watoa huduma wabadili mbinu na kaulimbiu zao, kwa kuwa wapo wanaume wenye zaidi ya miaka 50 ambao hushindwa kwenda kupata huduma hiyo kwa kuona aibu kwani watoa huduma wengi ni wadogo sana kiumri kwao “Badilikeni ili mfanikishe kampeni hii wekeni utaratibu watu wenye umri kutengewa sehemu yao ya tohara na kuwe na watoa huduma wenye umri sawa na wao”

Kaimu mganga mkuu wa Mpanda Dk. Limbu Mazoya anakiri kuwahamasisha wanawake kutofanya tendo la ndoa na wanaume wasiofanyiwa tohara kwa sababu za kiafya “Hamasa hii ni muhimu kwaajili ya kumkinga mwanamke asipate saratani ya shingo ya kizazi”

error: Content is protected !!