Zingatia haya kama unaamka ukiwa umechoka sana

HomeElimu

Zingatia haya kama unaamka ukiwa umechoka sana

Kama unaona kwamba unakosa usingizi na kuamka ukiwa umechoka sana basi jua unaumwa ugonjwa wa kukosa usingizi “Insomnia” ambapo mtu huchelewa au kukosa kabisa kupata usingizi wakati wa usiku na kuamka asubuhi akiwa na uchovu mwingi.

Sayansi inasema binadamu wa kawaida anatakiwa alale kuanzia masaa 7 mpaka 8, kama unaona unapata shida ya kuamka ukiwa umechoka na kutopata usingizi mapema basi haya ni mambo unayotakiwa kufanya na kutofanya:

Fanya haya

– Hakikisha unalala muda huo huo kila siku

– Hakikisha unalala sehemu yenye utulivu

– Zima vitu vya umeme kama taa na simu dakika 30 kabla hujalala

– Hakikisha unaoga kabla ya kulala na mazoezi ya pumzi

Epuka haya

– Epuka kulala hovyo mchana kwani usiku utasumbuka kupata usingizi

– Usivute sigara wala kunywa pombe usiku

– Epuka milo migumu wakati wa usiku

– Epuka kunywa kahawa masaa 4-6 kabla ya kulala

Kama bado utakua unapata usingizi kwa shida na kuamka ukiwa umelala basi ni vyema ukaenda hospitali kwa matibabu zaidi.

error: Content is protected !!