Mwalimu Mkuu akamatwa kwa udanganyifu mtihani darasa la 4

HomeKitaifa

Mwalimu Mkuu akamatwa kwa udanganyifu mtihani darasa la 4

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shimbale, Gaudensia Anyangi(45), amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la nne huku Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Shadrack Masiji akisema kuwa mwalimu huyo alikamatwa Oktoba 28 mwaka huu, saa 5:30 asubuhi.

“Aliwachukua wanafunzi wa darasa la tano na sita na kuwapeleka katika chumba cha mtihani ili wawafanyie mitihani wanafunzi wenzao wa darasa la ne ambao ni watoro, na tayari wanafunzi hao walikuwa wameshafanya mtihani wa Kiswahili na Hisabati. Lakini kwa bahati nzuri wasimamizi wa mtihani walifanikiwa kugundua hilo na kumkamata,” alisema Masiji.

Kamanda Masiji amesema kwa sasa upelelezi unaendelea na baada ya kukamilika jalada litafikishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua za sheria na kufikishwa mahakamani.

error: Content is protected !!