Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa Serikali ya Tanzania itaondoa sharti la kulipia viza ya kitalii kwa Raia wa Angola kuingia Tanzania, kama ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Angola ilivyoondoa sharti hilo kwa raia wa Tanzania kuingia Angola tangu mwaka jana, lengo likiwa ni kudumisha uhusiano kati ya mataifa haya mawili na kuongeza wigo wa sekta ya utalii, biashara na uwekezaji.
Rais Samia amesema hayo jana Aprili 08,2025 wakati yeye na mwenyeji wake Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço wakiongea katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya Luanda nchini Angola. Rais Samia yupo nchini Angola kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu na leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara hiyo.