Tetesi za Soka Barani Ulaya leo Septemba 20, 2021: Tchouameni, Kingsley, Pogba, Olmo, Lingard, Bailly, Koeman

HomeMichezo

Tetesi za Soka Barani Ulaya leo Septemba 20, 2021: Tchouameni, Kingsley, Pogba, Olmo, Lingard, Bailly, Koeman

Chelsea itakabiliana ana kwa ana na Juventus kupata saini ya kiungo wa chini ya umri wa miaka 21 wa Ufaransa na Monaco Aurelien Tchouameni, ifikapo dirisha dogo la usajili Januari. (Tuttomercatoweb – Italian)

Kiungo Jesse Lingard, 28, na beki Eric Bailly, 27, ni miongoni mwa wachezaji saba ambao wanaweza kuuzwa na Manchester United mwezi Januari. (Sun)

Liverpool, Tottenham na Juventus wamepania kupigania winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25. (Fichajes – Spanish)

Chelsea pia inavutiwa na Coman baada ya mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Bayern Munich kumtaka aondoke klabuni. (Mirror)

Mkataba wa Pogba na Manchester United utafikia kikomo majira yajayo ya joto, klabu hiyo imejiandaa kutoa ofa ya Pauni 400,000 kwa wiki kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara wa juu zaidi katika Ligi Kuu ya England wakati wote. (Express)

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman hajui hatma yake iko vipi wakati kukiwa na ripoti kwamba rais Joan Laporta anaunda orodha ya watu watakaochukua usukani wa klabu hiyo (Express)

Juventus walikuwa wamepanga kumsaini Gianluigi Donnarumma, 22, bila malipo kutoka AC Milan msimu huu wa joto, lakini walilazimika kujiondoa kwa sababu za kifedha, na kuiruhusu Paris St-Germain kumchukua (Goal)

Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo amepuuza maoni ya nyota wa Argentina Lionel Messi, 34, atapata zaidi ya pauni milioni 30 kwa msimu wakati wa mkataba wake wa miaka mitatu. (Mail)

Manchester United inawasiliana na kiungo wa England Jesse Lingard, 28, juu ya mkataba mpya. Bruno Fernandes na Luke Shaw pia wako kwenye ‘orodha ya wanaozingatiwa kwa mkataba’ na kilabu hiyo. (Fabrizio Romano)

Arsenal inaandaa dau la pauni milioni 20 kwa Winga wa Uholanzi mwenye chini ya umri wa miaka 21 na winga wa Club Bruges Noa Lang, 22. (Fichajes via Mirror)

error: Content is protected !!