Tetesi za Soka Ulaya leo Septemba 26 (Kante kuondoka Chelsea, Leno kutua Inter Milan)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Septemba 26 (Kante kuondoka Chelsea, Leno kutua Inter Milan)

Tottenham wanangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa kati Juventus na Sweden Dejan Kulusevski, 21(Mirror).

Manchester United bado wanamsaka mlinzi wa RB Leipzig na Ufaransa Nordi Mukiele, 23, kuwa kiungo wa safu ya nyuma-kulia wa klabu hiyo (Fichajes – Spanish).

Inter Milan imemuweka mlindalango wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 29 katika orodha ya wachezaji wanaowalenga kuwachukua (Fichajes – Spanish).

Chelsea wapo tayari kumuuza kiungo wa kati Mfaransa N’Golo Kante (30) msimu ujao (Fichajes – Spanish).

Arsenal watalazimika kulipa takriban pauni milioni 38.5 iwapo watataka kuingia Mkataba na mshambuliaji wa Morocco Youssef En-Nesyri, 24 (Mundo Deportivo – Spanish).

Juventus wanaripotiwa kuwa watamuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30 mwezi Januari huku klabu za West Ham, Everton na Newcastle zikimtaka (Sun).

Chelsea wanajiandaa kutuma ofa mpya kwa ajili ya winga wa Italia Federico Chiesa (23). Mchezaji huyo ana mkataba wa mkopo wenye kipengele cha kununuliwa katika klabu ya Juventus kutoka Fiorentina (Calciomercato – Italian).

Mlinzi wa Leicester City na Uturuki Caglar Soyuncu (25) ni mmoja wa wachezaji wanaotafutwa na Real Madrid (Defensa Central – Spanish).

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 25, alitaka kujiunga na Manchester United kabla ya kuhamia Stamford Bridge (Bild – German).

Mlinzi wa Leicester City na Uturuki Caglar Soyuncu, mwenye umri wa miaka 25, ni mmoja wa wachezaji wanaotafutwa na Real Madrid (DefensaCentral – Spanish).

error: Content is protected !!