Tetesi za Soka Ulaya leo Septemba 27 (Watkins kwenda Tottenham, Ronaldo kuinoa Man United)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Septemba 27 (Watkins kwenda Tottenham, Ronaldo kuinoa Man United)

Mshambulialiji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21 anayenyatiwa na Manchester City, anajiandaa kufanya mazungumzo mapya Fiorentina (DAZN, Manchester Evening News).

Chelsea inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus kumpata kiungo wa kati wa AS Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21 (Calciomercato – Italian).

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic ameitenga klabu hiyo na tetesi zinazowahusisha na usajili wa mchezaji wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger,28. (DAZN, Goal)

Mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins (25) ni miongoni mwa wachezaji wanaonyatiwa na Tottenham (Fichajes – Spanish).

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema ukosefu wa muda wa kucheza unaomkabili winga wa England Jadon Sancho, 21,”unaniumiza moyo” (Sport1, Express).

Tottenham ilikuwa na makubaliano ya kanuni kumsajili mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Uhispania Pau Torres (24) kutoka Villarreal msimu huu, lakini kiungo huyo “amependelea kusubiri ofa nzuri zaidi ” (AS – Spanish).

Cristiano Ronaldo anataka kustaafu akiwa katika klabu ya Manchester United. Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 36, pia anahitaji jukumu la ukocha katika klabu hiyo (Sun).

Chelsea wanajiandaa kuwasilisha dau la euro milioni 120 sawa na (£102m) kumnunua mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt (22) (AS – Spanish).

Manchester City wanapania kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig Mfaransa Christopher Nkunku, 23 (Fichajes, TEAMtalk).

Leicester City wameonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Lazio Mhispania Luis Alberto, 28 (Fichajes – Spanish).

Juventus wanaangalia uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Dortmund na ubelgiji Axel Witsel, 32 mwezi Januari mwakani (Calciomercato – Italian).

error: Content is protected !!