Kila mtu anatamani afikie ngazi fulani ya maisha. Iwe katika elimu, biashara au hata kazi, kunakuwa na matamanio fulani ya mtu kukua ili kufikia ndoto zake na ili aweze kupanda ngazi na kwenda kule anakotaka, anahitaji marafiki na watu wa karibu watakaomshika mkono na kumpa ‘support’ ya kila anachofanya.
Lakini wote hao hawatakua na maana yoyote kama hauna rafiki mmoja mwenye umuhimu mkubwa ambaye ni UWAJIBIKAJI. Rafiki huyu ni wewe mwenyewe.
Uwajibikaji ni pamoja na kuwa na nidhamu, kutumia muda vizuri na kujikosoa pale unapofanya makosa na kufurahia kile unachokifanya na kukipa umuhimu unaostahili.
Hivyo basi, Unatakiwa kuwajibika na maisha yako binafsi bila kusubiri watu wengine wakushike mkono na kukupeleka kule unakotaka.