Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema hadi kufikia Agosti 2021 ujenzi wa SGR kipande cha Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro ulikuwa umefikia 93.
Kadogosa ameyasema hayo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokagua ujenzi wa kipande hicho Septemba 12 mwaka huu na kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi wa usafirishaji wa bairia na mizigo kwa kupunguza muda wa safari kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na mikoa mingine kama Dodoma na Mwanza.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha pili cha mradi huo kinachoanzia Morogoro hadi Makutupola (Singida) ulikuwa umefika asilimia 70.11.
Amesema vipande vyote vya SGR vikikamilika vitachochea mpango wa serikali ya awamu ya sita katika kutekeleza seria ya viwanda na kufikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2025.
Mei mwaka huu Kadogosa alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 372.34 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha 5 cha reli ya Mwanza – Isaka chenye urefu wa kilometa 341 kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railways).