Kama uume wako umepinda ni jambo la kawaida kabisa, usijae taharuki ukadhani una tatizo la kiafya, kwani uume unaweza ukawa umepinda kuelekea juu, chini, kushoto au kulia, hii yote ni kawaida. Wataalamu wanasema haina madhara ya kiafya, uume ukiwa umepinda kwa nyuzi 30% au chini ya hapo hakuna tatizo, lakini zaidi ya hapo tunaweza kuanza kupata mashaka juu ya hilo na kuchukua hatua zaidi za uchunguzi wa kiafya.
Kwa muhtasari, uume wenye tabia zifuatazo hauhitaji tiba:
– Uume kama umepinda chini ya nyuzi 30
– Kama uume hauna maumivu, hasa wakati wa tendo la ndoa
Maumivu ya uume wakati wa tendo la ndoa ni jambo la kulichukulia kwa umakini mkubwa sana, kwani hizo ni dalili za kwanza kabisa za ugonjwa wa ‘Peyronies’. Huu ni ugonjwa ambao mwanaume hupata maumivu makali pale uume unaposimama, na ugonjwa huu sana huambatana na uume kupinda kama mwale wa mvua/upinde, na husababishwa na kupata kovu kwenye tishu za misuli ya uume.
Ugonjwa huu licha ya maumivu, lakini pia uume kuzidi kupinda kila siku, na unaweza kufikia hadi nyuzi 90, yaani kichwa cha uume kuangalia juu, chini. au pembeni kabisa na hivyo kumletea mtu shida kubwa sana wakati wa tendo la ndoa.
> Mtindo huu unaweza kusababisha uume kuvunjika wakati wa kujamiiana
Je, uume uliopinda ni bora wa kwenye ngono?
Wataalamu wa masuala ya ngono wanasema kuwa uume uliopinda unaweza kuwa bora kwenye ngono kulingana na aina ya mitindo/style wapenzi watakayotumia. Wakati wa ngono, mwanaume anatakiwa kugusa ‘G-spot’ ya mwanamke, sehemu ambayo ina hisia zaidi kuliko sehemu yeyote ile ya mwili wa mwanamke, hivyo kwa wanaume wenye uume uliopinda, hii ni rahisi kwao, lakini ni vyema kuzingatia uume wako umepinda kuelekea wapi.
Kama uume wako umepinda, iko mitindo ambayo inaweza kukusaidia kumfikisha kileleni mwenza wako mapema zaidi. Kama uume wako umepinda kuenda juu, basi ni vyema kama mwanamke atakaa juu kama vile yuko juu ya farasi, lakini kwenye hili lazima mwanaume awe makini kuepusha hatari zaidi kwenye uume. Lazima kuzingatia umbo na uzito wa mwanamke.
Na kama uume umepinda kuelekea chini, basi hapa hakuna budi mwanamke kuketi mtindo wa mbwa au watoto wa mjini wanasema mbuzi kagoma, nadhani tunaelewana kwenye hili. Lakini pia inawezekana uume umepinda kuelekea mashariki au magharibi, hapa hakuna budi wote mkalala ubavu, kisha uume upenyezwe mkiwa mmelalia ubavu, sasa hii itategemea ubavu wa kulalalia kulingana na kupinda kwa uume.
Lengo kubwa ni kuridhishana kwenye tendo, kikubwa ni mawasiliano baina ya wapenzi ili kufikia lengo na wote kulifurahia tendo la ndoa.