Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na DP World mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 900 hadi trilioni 1.8.
Msigwa ametoa takwimu hizo leo wakati akiziungumza na waandishi wa habari, kuhusu masuala mbalimbali ya nchi na uchumi pia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msigwa amesema pia Bandari ya Bagamoyo itaanza kujengwa Desemba mwaka huu.
Pia amegusia suala la kuongeza ndege ambapo amesema: “Tunaenda kuongeza ndege 8 kufikia 24., shirika letu la ndege linaimarika, tunaenda kuongeza vituo vya kimkakati 2050.


