Uwepo wa hewa na kemikali chafuzi kwenye maji na hewa kunaweza kuchangia mabadiliko ya uwiano katika kuzaliwa kwa watoto wa kike na watoto wa kiume. Utafiiti uliofanywa na PLoS Computational Biology nchini Marekani na Sweden umeonesha hivyo, ingawa bado haijathibitika katika ukamilifu wake kwamba kwa 100% hewa na kemikali hizo zinaweza kusababisha mabadiliko hayo.
Ingawa watafiti wanasaidiki kuwa katika viumbe wengine hali ya mazingira inaweza kuchangia jinsia ya mtoto kuwa ya kike au ya kiume, kwa mfano wadudu wengi watambaao pampoja na samaki, joto la mazingira yao linaweza kuathiri na kuchangia aina viranga/watoto kuwa na jinsia fulani.
Kwa wanadamu kumekuwa na ngano za miaka mingi ambazo hadi hivi leo bado hazina uthibitisho juu ya namna ambavyo mwanadamu anaweza kuchagua jinsia ya mtoto anayemtaka kwa kuzingatia aina ya vyakula fulani au mitindo na utundu katika kufanya tendo la ndoa, ingawa katika uga wa kisayansi bado haijathibitishwa kama kuna mazingira ya nje ya mwili wa mwanadamu yanayoweza kuchagua jinsia.
Utafiti unasemaje?
Kiwango cha uwiano wa kuzaliwa kati ya watoto wa kike na wakiume huitwa Sex Ratio at Birth (SRB), SRB ikiwa juu maana yake ni kwamba watoto wa kiume wanaozaliwa ni wengi zaidi, na kama SRB ikiwa chini maana yake ni kwamba watoto wa kike wanazaliwa wengi zaidi.
Utafiti uliofanywa nchini Marekani pamoja na Sweden ulioangazia kutazama uhusiano baina ya uchafuzi wa mazingira pamoja na hali za kisaikolojia kama mkazo na msongo wa mawazo kama vinaweza kuwa na mchango katika kuchangia kujua aina ya jinsi ya mtoto kabla ya mimba kutungwa. Utafiti huo uliiongozwa na Dkt. Andrey Rzhetsky katika Chuo Kikuu cha Chicago ulichukua rekodi za watoto milioni 6 na kulinganisha na taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa. Kati ya watoto milioni 6, taarifa za watoto milioni 3 zilitoka Marekani kati ya mwaka 2003 hadi 2011 na milioni 3 walitoka Sweden kati ya mwaka 1983 hadi 2013.
> Mbinu 10 za zitakazo kusaidia kupata watoto mapacha
Majibu ya utafiti
1. Majibu ya awali yalionesha hakuna uhusiano kati ya kiwango kikubwa cha kukosekana kwa ajira na matatizo mengine ya kiakili kama msongo wa mawazo, na kuchagiza aina ya jinsia ya mtoto.
2. Pia imegundulika kuwa zipo hewa na kemikali chafuzi ambazo zimechangia uwiano kushuka au kupanda katika kuzaliwa kwa watoto wa kike na wakiume. Imegundulika madini ya chuma (iron) pamoja na lead yamechangia kuongezeka uzao wa watoto wa kike, huku madini na kemikali kama Polychlorium biphenyls (PCBs), Mercury, Carbon monoxide, aluminium kwenye hewa, chromium na madini ya arsenic kwenye maji yameongeza uzao wa watoto wa kiume.
Kwenye hitimisho la utafiti huo imeonekana kwamba, kwa sasa si kwa 100% kuwa hewa na kemikali kwenye mazingira zinaweza kuwa taarifa za kuamika moja kwa moja kwenye kutoa tafsiri ya uwiano wa watoto wanaozaliwa kulingana na jinsia zao, bali huu ni mwanzo mzuri wa utafiti na pia ni taarifa itakayowasaidia watunga sera hasa kwenye kutunga sera mkakati katika utunzaji wa mazingira ambazo zinatasaidia ustawi wa binadamu katika mazingira yake.