Rais Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) umetekeleza lengo namba nne kwenye malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG’S).
Dk. Samia amesema hayo leo Alhamisi Januari 29,2026 akizindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Darasa la I na II.
Kwa mujibu wa Dk. Samia, lengo hilo namba nne linahimiza kufanya ubora wa elimu.
“Tumetekeleza mikakati yetu ndani ya Taifa, ndani ya Afrika, lakini pia kimataifa. Kwa hiyo Umoja wa Mataifa wakijua tulichokifanya leo watatupa pongezi nyingi sana, kwa haya tulioyafanya,”
“Ndugu zangu niseme, tupo katika njia sahihi na tunakwenda vizuri,” amesema Dk. Samia.


