Video za Tiktok kumfikisha Don Jazzy Zanzibar

HomeKimataifa

Video za Tiktok kumfikisha Don Jazzy Zanzibar

Mtayarishaji maarufu wa muziki, mtunzi wa nyimbo, mjasiriamali, na mfadhili na mmiliki wa lebo ya Mavins Records Don Jazzy ameweka wazi kwamba mwakani anatarajia kuja nchini Tanzania baada ya kuona video za vijana na watoto wakipiga mbizi eneo ya forodhani, Zanzibar.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa @YessJamal kiongozi wa wapiga mbizi, Don Jazzy aliandika kwamba “ni kweli nafikiria kuja na hii inabidi iwe mwakani”, baada ya watu kumshawishi atembelee eneo hilo.

Hivi karibuni video hizo za wapiga mbizi zimeonekana zinasambaa kwenye mtandao wa Tiktok na Instagram na kufanya watu wa mataifa wengine kutamani kwenda kutembelea eneo hilo ili kujionea wenyewe ni nini kinatendeka.

Don Jazzy pia ameonekana akiweka video hizo hivi karibuni kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuonesha kufurahishwa na kupendezwa na kile kinachofanyika na wapiga mbizi hao.

error: Content is protected !!