Watatu washikiliwa, kufukua kaburi la Albino

HomeKitaifa

Watatu washikiliwa, kufukua kaburi la Albino

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu watatu wa familia moja kwa madai ya kufukua mwili wa kijana mwenye ualbino, Heri Kijangwa aliyekuwa na umri wa miaka 45 na kutoweka naa jeneza pamoja na mabaki ya mwili wake.

Heri alifariki Julai 4 mwaka huu kutokana na ugonjwa wa saratani ya ngozi na kuzikwa Julai 7 katika kijiji cha Tandwa wilayani Lushoto mkoani Tanga. Oktoba 26 mwaka huu familia ya marehemu ilikuta kaburi limefukuliwa na watu wasiojulikana na wakachukua jeneza pamoja na mabaki ya mwili.

> Hiki ni kijiji mkoani Tanga ambacho makaburi yamefukuliwa na maiti kuibwa

Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Safia Jongo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema majina ya watuhumiwa yamehifadhiwa na uchunguzi unaendelea ili kubaini kama kutakuwa kuna watu wengine wameshiriki, tunataka kujua pia sababu za kufukua mwili na kujua wapi mabaki ya mwili yamepelekwa.

Kabla ya kufariki Heri alikua anachukua Shahada ya Uzamili ya Afya ya Jamii katika chuo kikuu cha Muhimbili huku akiwa amemaliza Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kimataifa na Teknolojia mwaka 2015.

error: Content is protected !!