Watoto Ibilisi 117 wanaswa Tanga

HomeUncategorized

Watoto Ibilisi 117 wanaswa Tanga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Sophia Jongo amesema Jeshi la Polisi mkoani Tanga limewakamata watoto 117 wanaojiita watoto wa ibilisi wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya KIhalifu na pia wamekamata bunduki 11 zilizotengenezwa kienyeji sambamba na kugundua kiwanda cha kutengeneza magobore.

“Operesheni ilipangwa kimkakati, kumekua na matumizi mabaya ya silaha hizo aina ya gobore katika misitu yetu, hivyo ikatulazimu kupanga mikakati kujua ni wapi zinapotoka,” alisema nakuongeza ;

“Tulifanikiwa kumkatama mtu mmoja mwanaume ambaye alikua na mtambo wa kutengeneza hayo magobore. Tulimkuta pia akiwa na magobore 11, mbali na magobore hayo pia alikua na vifaa vya kutengeneza silaha, kama trigger na cocking handle ambazo zinatumika katika silaha hizo,” alisema Jongo.
Aidha alisema katika operesheni hiyo , pia walikamata wahamiaji haramu 75, mawakala wao wanne na gari walilokuwa wakitumia kuwasafirisha wahamiaji hao.

error: Content is protected !!