Mtandao wa Whatsapp umesema upo kwenye majaribio ya kuweka mfumo mpya wa kusikiliza ujumbe wa sauti (voice note) ambao utamuwezesha mtumiaji kusikiliza ujumbe huo hata pale anapotoka kwenye “chat” yenye ujumbe huo.
Mfumo huu unakuja kuwarahisishia watumiaji wa mtandao huo ambao wengi hawakuridhishwa na namna ambavyo ujumbe wa sauti ulikuwa unajifunga pale unapofunga ‘chat’ moja na kuhamia nyngine hata kama haujamaliza kusikiliza hivyo kumlazimisha mtumiaji kubaki katika ‘chat’ hiyo mpaka mwisho wakati anaposikiliza.
Maboresho haya yatamuwezesha mtumiaji kuendelea kusikiliza sauti huku akifanya mambo mengine kwenye simu yake. Juu ya kioo cha simu itatokea mistari wa rangi ambayo inafanana na ‘audio player’ kuonesha jina na wasifu wa mtu aliyutuma sauti husika (voice message/voice note). #clickhabari