Serikali imefanya tathmini na kuainisha vituo vya afya kongwe 532 ambavyo vinahitaji kuongezewa na kukarabatiwa kwa miundombinu yake.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) anayeshughulikia afya, Dk Jafar Seif amesema hayo bungeni leo, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe aliyehoji lini serikali itakarabati kituo cha afya pamoja na nyumba za watumishi wa Kituo cha Afya Masama.
“Kituo cha Afya cha Masama kilijengwa Mwaka 1979 hali inayopelekea kuwa na miundombinu michache na chakavu.
“Kituo hicho kinahitaji miundombinu muhimu ikiwa ni pamoja na jengo la huduma za wagonjwa wa nje OPD, maabara, jengo la huduma za uzazi, jengo la upasuaji, jengo la kufulia, Kichomea taka, vyoo vya nje na nyumba za watumishi.
“Serikali imefanya tathmini na kuainisha vituo vya afya kongwe 532 ambavyo vinahitaji kuongezewa na kukarabatiwa kwa miundombinu yake.
“Aidha, jumla ya Sh bilioni 102.08 zinahitajika kwa ajili ya uboreshaji wa vituo hivyo. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya kongwe kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya Masama,” imesema.


