Ziara ya Rais Samia Marekani yajibu

HomeKitaifa

Ziara ya Rais Samia Marekani yajibu

Ubalozi wa Marekani nchini umesema ujumbe wa kampuni 19 kubwa za uwekezaji nchini Marekani utafanya ziara Tanzania kuona fursa za biashara na uwekezaji.

Taarifa ya ubalozi huo na Idara ya Huduma za Biashara ya Marekani imeeleza kuwa ujumbe huo utafanya ziara ya siku mbili Septemba 27 na 28.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kampuni hizo kwa pamoja zina uwekezaji wa zaidi ya Dola za Marekani trilioni 1.6.

“Ujumbe huo utaongozwa na Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano na matawi ya chama cha wafanyabiashara wa Kimarekani (AmCham) katika nchi za Kenya, Tanzania na Afrika ya Kusini, utalenga kuzitambulisha kampuni za Kimarekani kuhusu fursa zilizopo katika masoko ya Tanzania na Zanzibar,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa ilieleza kuwa ujumbe huo utakutana na kujadiliana na maofisa wa serikali za Tanzania/Zanzibar, utapokea taarifa kutoka ubalozi wa Marekani, utakutana na viongozi wa sekta binafsi ya Tanzania na kusikia uzoefu wa kampuni za Kimarekani zenye shughuli zao nchini Tanzania.

error: Content is protected !!