Zijue faida za kula chakula cha usiku mapema

HomeElimu

Zijue faida za kula chakula cha usiku mapema

Adeline Munuo, mtaalamu wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFCN), ameeleza kuwa mtu anayekula usiku muda mfupi kabla ya kulala hujiweka katika hatari ya kuongezeka uzito kwa sababu mwili unakuwa katika hali ya mapumziko hivyo hushindwa kumeng’enya chakula ipasavyo.

Munuo amefafanua kwa kueleza kuwa “matokeo ya mwili kushindwa kumeng’enya chakula vizuri hupelekea mabaki ya chakula kubadilishwa kwenda kwenye mafuta na kuhifadhiwa hivyo kuchangia kuongeza uzito wa mwili.”

Aidha ameeleza kwamba usiku ni muda ambao mwili hufanya kazi nyingine ikiwemo kutengeneza seli zilizoharibika hivyo mwili hushindwa kufanya kazi hii endapo utakuwa unashungulikia mmeng’enyo wa chakula hivyo kuuweka katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa kiurahisi.

Kwa mujibu wa Munuo, ili kuwa na afya bora ni muhimu mtu ale angalau saa mbili kabla ya muda wa kulala.

error: Content is protected !!