Mange Kimambi amepotea njia

HomeKitaifa

Mange Kimambi amepotea njia

Na Isaya Mdego, safarini Marekani.

Jana na usiku wa kuamkia leo Mange Kimambi amechapisha maandiko mawili ya kumtukana Rais Samia Suluhu. Wako waliomsifia kwenye sehemu ya maoni ya maandiko hayo wengi wakitumia majina ya kificho lakini wako wengi waliomkemea kwa kukosa staha. Wengine wamekwenda mbali zaidi na kusema huenda Mange amenunuliwa na wabaya wa Rais Samia kufanya hivyo.

Mimi nitajikita katika mambo matatu.

Moja, mimi ni moja ya watu wanaoamini kwa dhati Mange anahitaji msaada wa tiba ya akili. Katika jamii ya watu wenye akili timamu hakuna mtu anayeweza kuamua kuishi kwa kuuza picha za uchi za binadamu wengine. Mtu wa namna hii ni hayawani, kichaa na anayehitaji msaada wa tiba ya akili. Tukio hili la Mange ni mwendelezo wa matukio ya kuwakumbusha wale wanaomshangilia kwamba wanadili na mwehu anayehitaji msaada.

Pili, alichokifanya kinanyooshea vidole baadhi ya wanasiasa na watu mashuhuri. Wengi wetu tunafahamu kwamba Mange yuko karibu na baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali, wanasiasa nchini na baadhi ya wafanyabiashara na wapo kati yao ambao wamekuwa wakimpa fedha ama feva fulani fulani ikiwemo tukio la kuwezesha kupata pasi yake mpya ya kusafiria. Katika hali ya kawaida baadhi ya watu wanajiuliza, je inawezekana ametumwa? Na nani? Kwa lengo gani hasa? Itafahamika baada ya muda.

Tatu, iwe ametumwa au la, nadhani bado hajaelewa Rais Samia ni mtu wa namna gani. Kama si jambo linalohusu maisha ya wananchi basi huwa halimtetereshi. Rais ana masikio na vyombo kila kona ya nchi, anajua tunalala na kuamka vipi popote Tanzania. Katika moja ya chapisho lake Mange kazungumzia maji na umeme (huenda hafahamu kwamba matatizo haya yamepungua kwa kiasi kikubwa), kasemea NHIF (huenda pia hajui kwamba NHIF imeelemewa baada ya Serikali kuanza kuchukua mikopo toka kwake mwaka 2016 bila kulipa), kasema wanawake wanajifungua kwa shida (ni kama hajui kwamba siku hizi kila hospitali ya wilaya ina wodi mpya ya wazazi na karibu kila kitu cha afya nchini kina huduma hiyo). Sababu zake ni kama kaokoteza ili kuweza kuweka wasilisho lake.

Huenda anadhani Rais Samia atasema “asakwe” kama enzi za JPM ama alipwe, nadhani tujiandae kwa surprise sababu ninamvyosoma Rais Samia sio wa hivyo. Ataendelea kupiga kazi na kukupuuza kama vile haupo. Tuipe muda Mama atufunze siasa.

error: Content is protected !!