Tanzania ya kwanza Afrika, ya tano duniani kwa ongezeko la watalii

HomeKitaifa

Tanzania ya kwanza Afrika, ya tano duniani kwa ongezeko la watalii

Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN) kupitia takwimu zake za robo ya kwanza ya mwaka 2024 katika Ripoti yake ya World Tourism Barometer imeitaja Tanzania kama miongoni mwa nchi zilizofanya vizuri kwa kuongeza idadi ya watalii kimataifa.

Ripoti hiyo inaonyesha Tanzania ikiwa ya kwanza Afrika na tano duniani kwa kuwa na ongezeko la watalii asilimia 53 ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

10 Bora ya Dunia iko hivi: Qatar (+177%), Albania (+121%), Saudi Arabia (+98%), El Salvador (+90%), Tanzania (+53%), Curaçao (+45%), Serbia (+43%), Uturuki (+42%), Guatemala (+41%) and Bulgaria (+38%).

Kwa mujibu w aripoti hiyo, Tanzania imefanya vyema kwenye upande wa mapato ikiwa nafasi ya nne duniani kwa kufikia asilimia 62 ikilinganishwa na kipindi cha robo ya kwanza kabla ya Uviko mwaka 2019.

Nchi 10 Bora Duniani katika kipendele hiki ni: Serbia (+127%), Uturuki (+82%), Pakistan (+72%) Tanzania (+62%), Portugal (+61%), Romania (+57%), Japan (+53%), Mongolia (+50%), Mauritius (+46%) and Morocco (+44%).

Haya ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu iliyofanya katika kuhakikisha inatangaza vivutio vya kitalii vilivyopo nchini pamoja na kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani na utulivi ili watalii wengi zaidi waweze kuja.

Ikumbukwe, juhudi za Serikali zilizoleta ongezeko hilo la watalii ni pamoja na ushiriki wa Rais Samia Suluhu katika filamu ya Tanzania: The Royal Tour na sasa filamu mpya ya “Amazing Tanzania”.

error: Content is protected !!