10 Septemba siku ya kuzuia kujiua

HomeKimataifa

10 Septemba siku ya kuzuia kujiua

Nchini Marekani, mwezi Septemba ni maalum kuhakikisha unazuia mtu kujiua kwani wanaamini tunaishi katika nyakati ngumu hivyo mtu anaweza kuchukua maamuzi ya kukatisha uhai wake kwa namna moja au nyingine.

Zaidi ya watu 800,000 hufariki kila mwaka kwa sababu ya kujiua na hii ni sababu namba 10 ya vifo vinavyotokea ulimwenguni.

Mtu anachukua maamuzi ya kujitoa uhai baada ya kukosa tumaini, kutengwa na kuhisi kama mzigo. Ndiyo maana tunashauri kuwa karibu na ndugu, familia na marafiki ili kuondokana na hali hiyo.

Unawezaje kuzuia kujiua?

Imarisha uhusiano wa jamii na kuwa na mzunguko wa marafiki wenye upendo ili iwe rahisi kwako kupata msaada wa pale unapojihisi mpweke.

Hakikisha unapata tiba ya kisaiolojia. Tiba ni muhimu katika kupambana na ugonjwa wa akili na kuondoa mawazo ya kujiua.

 

error: Content is protected !!