Itakumbukwa kwamba msanii Juma Jux aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Vanessa Mdee.
Baadaye penzi lilivunjika, Vanessa akazama kwenye penzi na staa wa Marekani, Rotimi.
Jana Vanessa na Rotimi walionesha mitandaoni kwamba Vanessa ni mjamzito. Maneno ya mtandaoni hayakuachwa kuelekezwa kwa Jux, mashabiki wakitamani kusikia neno lake.
Jux amejibu, ametoa wimbo mpya (Sina Neno) ambao maneno yake yanaelekezwa kwa mwanamke ambaye sasa anayetarajia kupata mtoto kama ilivyo kwa Vanessa.
Sikiliza wimbo huo.