SGR yazidi uwezo wa Bandari ya Dar

HomeKitaifa

SGR yazidi uwezo wa Bandari ya Dar

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imetoa maazimio yake juu ya uwezo wa reli ya kisasa ya SGR ambayo inaizidi Bandari ya Dar es Salaam.

Kamati hiyo imesema changamoto ya SGR kutokupata mzigo wa kutosha kusafirishwa ni jambo litakalokwamisha kupatikana kwa tija ya uwekezaji uliofanyika na kwamba mkwamo huo utaweza kutatuliwa kwa kuwa kuongeza bandari ya Dar es Salaam na kujenga Bandari ya Bagamoyo.

Maazimio yaliyofikiwa ni, serikali iharakishe utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Serikali iharakishe zoezi la kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuongeza Gati za kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam na zoezi hilo likamilike kabla ya ujenzi wa Reli ya SGR kukamilika.

Pia, Kamati hiyo imesema endapo serikali itafanyia kazi maazimio hayo, itaisaidia SGR kupata mizigo ya kusafirisha hivyo kuleta tija iliyokusidiwa.

error: Content is protected !!