Rais Samia aagiza ujenzi wa Shule za ghorofa

HomeKitaifa

Rais Samia aagiza ujenzi wa Shule za ghorofa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, amesema ni vyema ujenzi majengo ya shule nchini ufanyikie kwa mtindo wa ghorofa ili kuepuka adha ya uhaba wa maeneo uliopo. Maelezo hayo aliyatoa Desemba 5 jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa barabara ya Mwenge-Morocco alipojibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba.

Mheshimiwa Rais Kinondoni tumepokea Sh. Bilioni 3.3 katika zile fedha za Covid kwa ajili ya kujenga madarasa, maeneo ya hospitali Kinondoni mimi nilihitaji shule mbili za sekondari, kata zangu mbili hazina shule ya sekondari, kata ya Tandale na kata ya Kinondoni”. Alisema Mhe Abbasi Tarimba.

Rais Samia alisema tatizo hilo alikutana nalo hata alivyoenda Mkuranga, na kusema kuwa sasa ni wakati wa kubadili mtindo wa ujenzi wa madarasa.“Na leo nalikuta sehemu ya pili, nilipokwenda Mkuranga nilikuta tatizo hili, ujenzi wa shule, lakini eneo halitoshi, nimelikuta tena hapa kinondoni, nadhani ni wakati mwafaka sasa tubadilishe ujenzi wa shule zetu, baada ya mabanda (majengo) kwenda kwa upana sasa yaende kwa juu (ghorofa), nadhani kwa eneo dogo tunalolipata tujenge kwa juu, ambako hakuna mipaka” alisema Mhe. Rais Samia Suluhu.

error: Content is protected !!