Shusho afunguka kashfa ya kunywa pombe

HomeBiashara

Shusho afunguka kashfa ya kunywa pombe

Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Christina Shusho, ameweka wazi kuhusu video inayomuonyesha akiwa anakunywa kinywaji kinachodhaniwa kuwa ni pombe.

Shusho amesema kwamba kile ni kinywaji wanachopewa watu wanaoheshimiwa au wageni kwenye sehemu waliyokwenda na sio pombe kama wengi walivyokuwa wakidhani. “Tulijua watu wangehisi ni kilevi, lakini kule tulipokuwepo kwa watu ambao wanawaheshimu hawawapi soda zetu hizi za shilingi mia tano.

Wanawatafutia vinywaji kama soda au juisi lakini ni zile zinazouzwa bei ghali kidogo,” alisema Shusho.Shusho alisema video zilirekodiwa kwa kupanga kwani walijua Watanzania watasema walikuwa wanakunywa pombe, huku akiongeza kwamba walirekodi video tatu za aina hiyo zikiwaonyesha wanakunywa hizo juisi zilizopo kwenye chupa kama za pombe.

error: Content is protected !!