Travis Scott afunguliwa kesi ya mauwaji

HomeElimu

Travis Scott afunguliwa kesi ya mauwaji

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Travis Scott amefunguliwa kesi ya kuchochea ghasia kwenye tamasha lake ambalo limesababisha vifo vya watu nane na mamia kujeruhiwa. Travis amefunguliwa kesi na mmoja wa shabiki yake, Kristian Paredes, ambaye naye ni muhanga wa tukio hilo aliyejeruhiwa katika tamasha la Astroworld lililoandaliwa na msanii huyo.

Tamasha hilo lililofanyika jijini Texas na kuhudhuriwa na maelfu wa mashabiki wa msanii huyo lilimalizika ghafla baada kuzuka moto na watu kuanza kukimbia hovyo kwa woga na taharuki. Baada ya tukio hilo la kutisha Travis amesema anajisikia vibaya kwa kilicho tokea na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Polisi na familia zilizoathirika na tukio hilo.

“Nimejisikia vibaya sana kwa kile kilichotokea, maombi yangu yapo pamoja na wale wote walioathirika na tukio hili. Naungana na Polisi wa Houston katika kusaidia kwa namna yoyote ile familia na jamii kwa ujumla,” ameandika Travis.

Katika video zinazosambaa mitandaoni zinaonyesha mashabiki wakipiga makelele kumshangilia Rapa huyo na wengine wakipaza sauti kuomba msaada jambo lililomfanya Travis kuchelewa kujua kilichokuwa kinaendelea.

error: Content is protected !!