Latra yatangaza nauli mpya za mwendokasi

HomeKitaifa

Latra yatangaza nauli mpya za mwendokasi

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli mpya za teksi mtandaoni, pikipiki mtandao na Mabasi yaendayo Haraka (BRT) maarufu mwendokasi ambayo imepanda.

Nauli za mabasi ya mwendokasi kwa njia kuu kwa safari ni Sh 750 kutoka Sh 650, njia mlisho Sh 500 kutoka Sh 400,njia mlisho ukijumlisha na njia kuu Sh 900 na njia ya Kimara kwenda Kibaha ni Sh 700.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluho alisema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14.

Pia, alisema walipokea mapendekezo mengine ya kupanda kwa nauli za wanafunzi kutoka Sh 200 mpaka Sh 300 lakini walikataa na kukubaliana ibaki Sh 200.

error: Content is protected !!