Rais Samia apongezwa na TUCTA kufanyia kazi vikokotoo

HomeKitaifa

Rais Samia apongezwa na TUCTA kufanyia kazi vikokotoo

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limesema kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu cha asilimia 33 kimelenga kumkomboa mtumishi wa umma.

Emmanuel Mwakajila, Mjumbe wa Baraza Kuu la TUCTA, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha dhamira hiyo ya dhati.

Pia baraza hilo limempongeza Rais Samia kwa kuwapa mafunzo kuhusu kikokotoo hicho kipya kuwajengea uelewa ili kufikisha elimu hiyo kwa wafanyakazi.

“Mtakumbuka Mei Mosi, mwaka huu, Rais Samia aliwatangazia wafanyakazi kwamba amekubali ombi la wafanyakazi kufikia kikokotoo cha asilimia 33 wanapostaafu na kuachana na kile cha zamani cha asilimua 25,”alisema.

Pamoja na mabadiliko hayo, Mwakajila alisema kumeibuka upotoshaji ambao umezagaa kwamba kikokotoo hicho kitanyonya haki za wafanyakazi wa sekta binafsi na watumishi wa umma.

“Mafunzo haya yaliyotolewa yameonyesha dhamira njema ya serikali iliyopo madarakani ya kuhakikisha mtumishi anapostaafu kila mwisho wa mwezi atakuwa anapokea kiasi kikubwa cha pensheni, tofauti na kikotoo cha asilimia 25.

“Hii inaweka uhakika wa maisha ya mfanyakazi baada ya kustaafu. Kwa muda mrefu vikokotoo hivi vilikuwa havitendi haki kwa maana, kikokotoo cha zamani cha asilimia 25 kilikuwa kinawapa faida watu wachache ambao walikuwa wakipata asilimia 50,” alisema Mwakajila.

 

error: Content is protected !!